Search This Blog

Tuesday, November 17, 2020

Taifa Stars kuvaana na Tunisia leo

 

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeendelea na maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa marudiano dhidi ya Tunisia unaotarajiwa kupigwa leo Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Stars inaburuza mkia kwenye msimamo wa Kundi J katika michuano ya kufuzu Afcon 2022, ikiwa imekusanya pointi tatu kwenye michezo mitatu, wakishinda dhidi ya Guinea ya Ikweta na wamepoteza dhidi ya Libya na Tunisia ambao ndiyo vinara wa kundi.

 Tunisia walikusanya pointi tatu juzi na kufikisha 9, baada ya kuichapa Stars bao 1-0 nchini Tunisia.

Sasa Stars inatakiwa ishinde leo Jumanne ili kupata matumaini ya kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazofuzu kutoka katika kundi hilo. Hadi sasa timu tatu zimefungana pointi na kila timu ipo katika nafasi yake kutokana na kigezo cha matokeo yalikuwaje timu zilizofungana pointi zilipokutana ‘head to head’

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yakifanyika Stars inaweza kuibuka na ushindi mbele ya Watunisia leo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...