Syria imelaani kwa matamshi makali ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo kwenye milima ya Golan ikisema hicho ni kitendo cha uchokozi kabla ya rais Donald Trump kuondoka madarakani.
Taarifa iliyotolewa na serikali mjini Damuscus imesema Syria inaitaka jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kulaani ziara hiyo ya kichokozi na inayokiuka sheria za kiamtaifa.
Ziara ya Pompeo kwenye maeneo ya makazi ya walowezi wa kiyahudi yalio kwenye ukingo wa magharibi pamoja na milima ya Golan ndiyo ya kwanza kuwahi kufanywa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.
Milima ya Golan ilikuwa sehemu ya Syria hadi Israel ilipolikamata eneo hilo kwenye vita vya mwaka 1967 na tangu mwaka 1981 inalikalia kwa mabavu.
Juhudi za Syria za kurejesha eneo hilo chini ya himaya yake zimegonga mwamba na rais Donald Trump alitangaza mwaka uliopita kutambua eneo hilo la ardhi kuwa milki halali ya Israel.

No comments:
Post a Comment