Baraza la Seneti la Marekani limeidhinisha uteuzi wa James Story kuwa kama balozi wake nchini Venezuela.
James Story amefahamishwa kwamba atahudumia wadhifa wake wa ubalozi wa Marekani huko Caracas akiwa katika mji mkuu wa Bogota nchini Colombia.
James Story anatabiriwa kuchukuwa majukumu muhimu kwa ajili ya kuongoza sera za Marekani nchini Venezuela katika kipindi cha utawala wa Rais mteule Joe Biden.
Mahusiano kati ya Marekani na Venezuela yalianza kuharibika kipindi cha uongozi wa Rais wa zamani wa Venezuela Hugo Chavez.
Tangu mwaka 2010, Marekani na Venezuela hawakuteua mabalozi wa pande zote mbili.
Nchi hizo mbili zilivunja mahusiano ya kidiplomasia kati yao mwaka jana na kuwaondoa wanadiplomasia wao baada ya utawala wa Washington kumuunga mkono Juan Guaido ambaye ni Rais wa Bunge la Kitaifa linaloongozwa na upinzani nchini Venezuela, na kujitangaza kuwa "rais wa mpito".

No comments:
Post a Comment