Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

Serikali ya Ethiopia yatangaza kuendeleza operesheni dhidi ya TPLF


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ametangaza kuwa operesheni ya kijeshi dhidi ya vikosi vya waasi vya Tigray People's Liberation Front (TPLF) kaskazini mwa nchi hiyo imefikia hatua za mwisho.

Katika taarifa aliyotoa kupitia akaunti yake ya mitandao ya kijamii, Ahmed alisema kuwa mudai wa siku 3 uliopewa vikosi vya TPLF vinavyoongoza jimbo la Tigray umekwisha, na operesheni hiyo itaendelea hadi hatua ya mwisho.

Akiwashukuru wanamgambo waliojisalimisha kwa jeshi la kitaifa la Ethiopia, Ahmed alibainisha kutokana na uamuzi wa kujisalimisha, watu hao wameweza kuokoa maisha yao kwa kuwajibika na kutii sheria.

Kwa upande mwingine, Mwanasheria Mkuu wa Ethiopia alitangaza kuwa akaunti za benki za kampuni 34 zinazohusiana na TPLF zimezuiwa.

Kikosi cha anga cha Ethiopia kiliendesha shambulizi la anga katika mji wa Mekelle ambao ni mji mkuu wa jimbo la Tigray hapo jana, kuwa kujibu mashambulizi ya roketi ya TPLF yaliyotekelezwa Amhara na Eritrea.

Waziri Mkuu Ahmed aliwahi kuzungumza kwenye televisheni ya kitaifa wiki iliyopita na kutoa wito wa kujisalimisha kwa vikosi vya TPLF.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...