Search This Blog

Thursday, November 5, 2020

Rais wa Malawi Chakwera aamuru bodi ya mitihani ivunjwe baada ya mitihani kusambaa mitandaoni



Rais Lazarus Chakwera ameagiza kuvunjwa kwa Bodi ya Mitihani baada ya mitihani ya Kitaifa ya mwaka huu kusambaa katika Mitandao ya Kijamii kabla ya Watahiniwa kuifanya.


Mitihani ya Sekondari nchini humo ilipangwa kuanza Oktoba 27 lakini imeahirishwa, hali iliyoleta ghasia za Wanafunzi kuandamana na Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.


Ikielezwa kuwa Polisi wamewakamata takribani Wanafunzi 38 na Walimu watatu kwa kukutwa na karatasi sita za Mitihani zilizosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...