Search This Blog
Sunday, November 1, 2020
Polisi yatoa onyo wanaotaka kuandamana
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Liberatus Sabas, amesema kuwa jeshi la polisi halitamvumilia mtu yeyote awe kiongozi wa chama au mfuasi, atakayefanya maandamano batili na kama kuna yeyote ambaye hakuridhika na matokeo afuate taratibu za kisheria kudai haki zao kama zipo.
CP Sabas ametoa kauli hiyo hii Oktoba 31,2020, na kuwasihi akina mama kuongea na watoto wao kwamba, wasithubutu kushiriki katika maandamano hayo na wasije wakarubuniwa na watu ambao hawana nia nzuri na Taifa.
"Nasisitiza kwamba jeshi la polisi halitakuwa na simile kwa yeyote atakayejihusisha na chokochoko hizi ambazo tunaziona zinaanza kuanzishwa na watu hawa ambao hawalitakii mema Taifa hili, nawaomba akina mama mkanye mwanao kwa sababu mwisho wa siku mtoto atakapopata matatizo atakulilia mama, sasa kabla matatizo hayajamfika nakuomba mkanye mwanao", amesema CP Sabas.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment