1. Kila waziri aijue wizara na Taasisi zake kwa kuzitembelea.
2. Kila Waziri atengeneze Mpango kazi na Bajeti kwa kutumia ilani, hotuba ya Rais, ahadi za kampeni, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar na kupata maoni ya Wadau wa wizara.
3. Kutembelea miradi yote ya wizara kwa kuangalia ubora, utaratibu wa zabuni, malipo yaliyofanyika na muda wa kumaliza.
4. Uwajibikaji wa Watendaji. Kila mtu awajibike kwa kazi aliyopewa na Huduma zitolewe kama zinavyotakiwa.
5. Kuhakikisha haki za watu zinatolewa, Wafanyakazi walipwe posho zao fedha za safari overtime walipwe pale wanapostahiki, haki za wananchi zitolewe na Watu wasikilizwe .
6. Utawala bora, Rushwa ubadhirifu uondolewe, Wizi wa makusanyo na fedha za bajeti na Matumizi mabaya ya Fedha za miradi.
7. Ukusanyaji wa mapato ya Serikali ZRB na TRA ziangaliwe.
8. Ubunifu; kila mtu abuni mambo mapya katika kazi, asisuubiri kuelekezwa, Tumia wataalamu waliopo kuleta ubunifu.
9. Urasimu uondoe usumbufu katika kupata huduma, Njoo kesho njoo kesho iondoke, Wananchi wapate majibu na mambo yenye maslahi ya Umma yasicheleweshwe.
10. Mawaziri wawe wepesi wa kuleta mapendekezo ya sheria pale ambapo sheria ni kikwazo.
11. Taarifa zinazofanywa zitolewe kwenye vyombo vya habari na mawaziri wawe marafiki na waandishi wa habari.
12.Wasikilize malalamiko ya watu. Kila wizara iwe na utaratibu wa kusikiliza malalamiko ya watu na kutumia teknolojia kutekeleza hili kama vile mitandao ya kijamii.
13. Kuhakikisha maeneo ya kufanyia kazi yanakuwa katika Mazingira mazuri ya kufanyia kazi, Mji wetu ni mchafu hakuna hata sehemu moja ambayo tunasema hapa afadhali, itafutwe njia mbadala ya kubafilisha hali hii.

No comments:
Post a Comment