Hivi ndivyo unaweza kusema kuwa ni Mafuriko ya wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Mbunge wao Mhe.Miraji Mtaturu walivyompokea kwa shangwe na furaha baada ya kuwasili katika Jimbo hilo la Singida Mashariki akitokea bungeni Dodoma kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumuani tena miaka mitano tena kwa ushindi wa kishindo.
Akizungumza na baada ya kupokelewa na wananchi wake na Chama cha CCM Mhe.Mtaturu amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kuendelea kumuamini tena huku akisema kuwa atawatumikia wananchi bila kuwabagua kwa itikadi zao za kisiasa.
Aidha Mtaturu amewambia wananchi kuwa uchaguzi kwasasa umekwisha hivyo wananchi washirikiane kuhakikisha Wilaya ya Ikungi inapata mafanikio na yeye kama kiongozi wao atawatumikia wote bila ubaguzi.
“Tayari Mimi ni Mbunge wenu nipo tayari kushirikiana nanyi, lakini pia tujenge mahusiano, tuachane na itikadi zetu za kisiasa sasa tujenge uchumi wa Jimbo la Ikungi, tumechelewa sana,”amesisitiza
Hata hivyo Mhe.Mtaturu ametaja vipaumbele saba atakavyoanza navyo ikiwemo suala la elimu ambapo atasimamia kuhakikisha watoto wanapata elimu bora,Maji,Umeme,Afya pamoja na miradi iliyopo inatekelezwa na kuibua mingine.
Aidha Mhe.Mtaturu amewahamasisha akinababa kuunda vikundi vya wakulima ili waweze kupata mikopo itakayosaidia kuinua kilimo chao katika wilaya ya Ikungi na pia wataweza kupata mikopo wakiunda vikundi hivyo.

No comments:
Post a Comment