Maafisa nchini Afghanistan wamesema wanajeshi 31 wameuwawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kuishambulia kambi ya kijeshi nchini humo, katika moja ya shambulio baya zaidi kutokea katika miezi ya hivi karibuni lililowalenga maafisa wa usalama.
Shambulio hilo limetokea nje kidogo ya mji wa Ghazni unaoshuhudia mapigano ya mara kwa mara kati ya Kundi la Taliban na vikosi vya serikali.
Kulingana na Baz Mohammad Hemat, mkurugenzi wa hospitali ya Ghazni, wamepokea miili 31 na watu wengine 24 waliojeruhiwa vibaya.
Msemaji wa wizara ya ndani ya Afghanistan Tariq Arian amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga aliliripua gari lililojaa vilipuzi mjini Ghazni bila ya kutoa maelezo mengine zaidi. Hakuna kundi lolote hadi sasa lililokiri kuhusika na shambulio hilo.

No comments:
Post a Comment