Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

Mchungaji milionea aiomba dunia iingilie kati kesi dhidi yake


Nabii milionea Shepherd Bushiri ametuma ujumbe kwa Jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika SADC, Bara la Afrika na dunia nzima akidai iingilie kati katika kesi inayomkabili yeye na mke wake nchini Afrika Kusini.

Nabii huyo ambaye ni raia wa Malawi pamoja na mke wake Mary wanashitakiwa kwa makosa 419 ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha Afrika kusini.

Katika ujumbe wake Nabii huyo maarufu, amesema kuwa kesi yake haiwezi kuendeshwa kwa haki nchini Afrika kusini, kutokana na kauli alizozitoa Waziri wa ndani wa Afrika Kusini Dkt Aaron Motsoaledi alizozitoa kwa kamati ya bunge Jumanne kuhusiana na kanisa lake.

'' La kusikitisha ni kwamba waziri alizungumzia kesi yetu inayotarajiwa kufanyika pamoja na michakato iliyopo ndani ya wizara ambayo ana mamlaka nayo, waziri aliieleza tume kuhusU mchakato ambao unatumiwa na idara yake wa kuwafuatilia watu wanaoingia na kuondoka Afrika Kusini na mchakato unaofuatwa na idara katika utoaji wa vibali'', ulisema ujumbe wa Nabii Bushiri.

Nabii Bushiri anasema: ''Hii ni moja ya michakato ambayo mimi na mke wangu tunapaswa kuifuata wakati imeingiliwa na mahakama ya juu nchini Afrika Kusini, ambayo pia waziri ameashirika kuwa alisikitika wakati haki zetu zilipolindwa na mahakama.''

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Nabii Bushiri anasema Waziri wa mambo ya ndani alisema kuwa kibali chake na cha mkewe si vya kudumu kuishi Afrika Kusini ni vya muda mfupi kwa hivyo kuishi kwao nchini humo ni ukiukaji wa sheria kwasababu ''mimi na mke wangu hatukuwasilisha taarifa stahiki kwa idara yake ili kutoa vibali, wizara yake ilitoa vibali vya kuishi kimakosa, na hivyo kuamua kufuta vibali hivyo'', imesema taarifa ya Nabii Bushiri kwa dunia.

Kulingana na maelezo yake, Nabii huyo ambaye ni raia wa Malawi anadai mchakato huo wa wizara ya mambo ya ndani tayari umemuhukumu kabla hajawasilisha maelezo yake kuhusu ni kwanini vibali vyao havipaswi kufutwa kwasababu hawakufanya kosa lolote, anasema.

''Waziri alisema kuwa mimi na mke wangu tunamiliki paspoti tano tofauti kila mmoja wetu. Anataka kuonesha kuwa hizi ni paspoti zenye majina tofauti na maelezo mengine, hili ni suala lililopo katika mahakama ya juu ya Afrika Kusini''

Anadai kauli ya Waziri inampa hofu kubwa kuwa hatapata kesi ya haki nchini Afrika Kusini.

Anasema anataka kesi yake na mkewe ifanyike nchini Malawi :''Ninaimani na Katiba ya Malawi kwasababu inawalinda raia wake wote ikiwa ni pamoja na mimi na mke wangu''.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...