Search This Blog

Saturday, November 21, 2020

Mazungumzo ya Brexit yasimamishwa kwa Covid-19


Mazungumzo ya Brexit yanayohusu EU na Uingereza yametangazwa kusimamishwa kwa muda baada ya mmoja wa wawakilishi kukutwa na virusi vya Corona (Covid-19).

Msimamizi wa mazungumzo ya Brexit wa EU Michel Barnier, alitoa maelezo kupitia mtandao wa kijamii na kufahamisha kusimamishwa kwa mazungumzo ya makubaliano yanayolenga kuboresha uhusiano wa kibiashara kati yao na Uingereza.

Barnier alisema, 

"Mmoja wa wawakilishi wa upatanishi kwenye timu yetu amekutwa na covid-19. Timu yetu ya wawakilishi pamoja na uoande wa David Frost tumechukuwa uamuzi wa kusimamisha mchakato wa mazungumzo ya Brexit ya Uingereza kwa muda mfupi." 

Frost alizungumzia suala hilo kupitia mtandao wa kijamii na kusema, 

"Nawasiliana na Michel Barnier na kufuatilia kwa makini hii. La muhimu ni hali njema ya kiafya kwa timu yetu. Nashukuru baraza la EÜ kwa masaada wa dharura."



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...