Makaburi matano ya halaiki yamepatikana katika mji wa Terhune uliowahi kukombolewa mwezi Juni kutoka mikononi mwa wanamgambo wa kundi la silaha linaloongozwa na Khalifa Hafter nchini Libya.
Msimamizi wa Idara ya Habari ya Timu ya Utafutaji iliyoko chini ya serikali ya Libya, Abdulaziz Jaferi, aliarifu kupatikana kwa makaburi matano ya halaiki katika eneo la Rabit mjini Terhune.
Akifahamisha kufukuliwa kwa miili ya maiti 4 hadi kufikia sasa, Jafer aliongezea kusema kuwa shughuli ya uchimbaji na utafutaji bado inaendelezwa kwa ushirikiano wa wataalamu wa masuala ya afya katika eneo hilo.

No comments:
Post a Comment