Search This Blog

Sunday, November 1, 2020

Macron amtuhumu Erdogan kwa kuchukua msimamo mkali kwa washirika wa NATO

 


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameituhumu Uturuki kwa kuchukua msimamo mkali kwa washirika wa nchi hiyo katika muungano wa kujihami wa NATO akisema kwamba nchi zinastahili kuzungumzia matatizo waziwazi. 

Katika mahojiano na shirika moja la habari la Kiarabu jana Macron amesema anapendelea kurejesha mahusiano kuwa mazuri ila Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan anastahili kuuheshimu Umoja wa Ulaya na Ufaransa na kujizuia kutoa matamshi ya kizushi. 

Erdogan na Macron walizozana baada ya kiongozi huyo wa Uturuki kutoa wito wa kususiwa kwa bidhaa za Ufaransa kama jawabu la Macron kutetea uhuru wa kujieleza kwa maana ya vibonzo vilivyochapishwa katika gazeti moja nchini humo vikimuonyesha mtume Mohammed jambo ambalo Waislamu wanasema ni kejeli na kumkosea mwenyezi Mungu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...