Search This Blog

Friday, November 27, 2020

Kituo cha udhibiti cha jeshi la kitaifa SMO chashambuliwa Syria


Watu 2 wameripotiwa kufariki na wengine 2 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa kwenye kituo cha udhibiti cha Jeshi la Kitaifa la Syria (SMO) kwa kutumia gari lililotegwa bomu wilayani Rasulayn, kaskazini mwa Syria.

Shambulizi hilo la kigaidi lilitekelezwa katika kituo cha ukaguzi cha SMO kwa kutumia gari lililotegwa bomu la gari katika kijiji cha Tel Jeneb mjini Mebruke kusini mwa wilaya ya Rasulayn.

Wanajeshi 2 wa SMO walipoteza maisha na wengine 2 wakajeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Hatima ya dereva wa gari hilo la bomu lililotumiwa kutekeleza shambulizi haijulikani.

Vikosi vya usalama vya ndani ya nchi vilianzisha uchunguzi juu ya shambulizi hilo na kubainisha kuwa kuna uwezekano lilitekelezwa na kundi la kigaidi la YPG / PKK.

Wilaya ya Rasulayn ilikombolewa kutokana na ugaidi kufuatia Operesheni ya Amani ya Jeshi la Uturuki iliyoendeshwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2019.

Kund la YPG / PKK ambalo linaendeleza uvamizi wa maeneo ya Ayn Isa na Tel Temir, limekuwa likitekeleza mashambulizi ya kigaidi mara kwa mara yanayolenga raia wa Rasulayn na Tal Abyad.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...