Search This Blog

Friday, November 20, 2020

Kinondoni yaanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhusu wamachinga


Mkuu wa Wilaya  Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo kwakushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, wameahidi kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Magufuli yakutaka kundi hilo lipewe kipaumbele katika kutimiza shughuli zao.

Akizungumza na wajasiriamali hao wasoko la Bunju B leo, Mhe. Chongolo amesema kuwa Serikali iliyopo madarakani iko mstari wa mbele kuhakikisha inaboresha mazingira ya wafanyabiashara na wajasirimali wadogowadogo ili waweze kutekeleza majukumu yao bila changamoto yeyote.

Jumatatu Oktoba 17,saa tatu asubuhi Mgombea Urais, wa Chama Chamapinduzi CCM Dk. John oseph Pombe Magufuli alisimama hapa, kweli sio kweli, na alizungumza masuala kadhaa ikiwemo  la Wamachinga kweli sio kweli, na aliahidi atasimamia masilahi ya wamachinga katika Wilaya hii, kweli sio kweli, sasa nasisitiza kwamba tunayafanyia utekelezaji” amesisitiza Mhe. Chongolo

Ameongeza kuwa  Mkuu wa Wilaya kama msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali zihusuzo ulinzi na usalama wa raia wake ameahidi kushughulikia changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kulinda ulinzi na usalama wa mali pamoja na biashara zao.

 “ Kiongozi Mkuu wa Serikali ndani ya Wilaya ya Kinondoni ni Mkuu wa Wilaya, sasa  mbona mnaniambia habari ya kuhama kuhama, nani kasema kwamba atawahamisha hapa, hatuwezi kuwahamisha, lakini pia mmesema mko tayari kutafutiwa eneo la karibu,hilo jambo litafanyika kwa haraka” amesema Mhe. Chongolo.

Awali  akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya huyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bunju B, Athuman Njama amesema kuwa aneo ambalo wajasiriamali hao wanafanyashughuli zao kwa sasa ni rafiki kwa sababu linafikika tofauti na eneo ambalo walitakiwa kwenda.

Katika hatua nyigine, Mhe. Chongolo amewataka kuzingatia suala la usafi  katika eneo ambalo wanafanya shuguli zao ili kuweka mazingira safi kwa watu ambao wanakuja kununua bidhaa katika eneo hilo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...