Search This Blog

Sunday, November 1, 2020

Kimenuka...Mbowe, Wenzake Mbaroni Tuhuma Kupanga Maandamano



KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kupanga maandamano.


Viongozi wa Chadema wanaowashikilia ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, Godbless Lema, Isaya Mwita (aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam) na Boniface Jacob aliyekuwa Meya wa Ubungo na mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa

wamepanga kuanza maandamano kitaifa yasiyokuwa na kikomo kuanzia Novemba 2, mwaka huu kwa kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta

Aidha, jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wanaowashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo polisi wamesema ni ya vurugu kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi. Wengine wanaosakwa ni viongozi wa chama cha ACT Wazalendo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...