Search This Blog

Sunday, November 8, 2020

Kidato cha Pili Kuanza Mitihani wa Kitaifa Leo


Wanafunzi wa kidato cha pili wapatao  646,148 kote nchini  wanatarajia kuanza Mitihani hiyo leo hadi Novemba 20, 2020. Kati yao 301,831 (46.71%) ni Wavulana huku 344,317 (53.29%) wakiwa Wasichana.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema idadi hiyo ni ongezeko la 5.7% ikilinganishwa na waliofanya mitihani hiyo mwaka jana.

Aidha, ameeleza kuwa Mitihani ya Darasa la Nne itafanyika Novemba 25 na 26, ambapo idadi ya Wanafunzi waliosajiliwa ni 1,825,679 wakiwemo Wavulana 909,068 na Wasichana 916,611.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...