Search This Blog

Monday, November 23, 2020

Jumuiya ya wazazi Ccm kuja na Mikakati ya Kuinua Elimu

 


Na John Walter, Manyara

Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi (CCM) imeeleza kuwa imejipanga kuanzisha shule za sekondari ambazo zitalenga kuwasaidia watoto na kuongeza mapato katika jumuiya hiyo ili iweze  kujiendesha vizuri.

Akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Manyara Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Dkt. Edmud Mndolwa,  alisema awali Jumuiya hiyo ilikuwa na shule lakini hazikuwa nzuri kutokana na muongozo kuwa mbaya.

"Tuna kila sababu ya shule zetu kufanya vizuri kinachotakiwa ni kuwa na adabu na kufuata miongozo iliyopo hakuna usimamizi wowote uliofanikiwa bila kuwepo na adabu" alisema Mndolwa.

Mndolwa alisema mtu ambaye hatakubaliana na miongozo ya uendeshaji shule hizo watamuondoa mapema na pia ikitokea mtu akagundulika ni mbadhirifu wa fedha atashughulikiwa.

Alisema kwa sasa kitega uchumi cha Jumuiya hiyo ni shule pamoja na ufugaji wa nyuki na watahakikisha wanakuwa na shule bora katika kanda nane ambapo watahakikisha wanafuta daraja la nne  na kubaki na daraja la kwanza  kwa asilimia 80 na daraja la pili asilimia 20.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi  Mkoa wa Manyara Fratern Kwaison alisema kuwa kama Jumuiya hiyo inahitaji shule  kuna haja ya kuanzisha kuanzia mwanzo na siyo kuchukua shule zile ambazo zilishaanzishwa baadaye zikachukuliwa na serikali. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...