Search This Blog

Monday, November 2, 2020

Israel yaanza majaribio ya chanjo ya COVID-19 kwa binaadamu


 Israel imeanza jaribio la chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID, ambapo kama itafanikiwa itaanza kutumiwa na umma mwishoni mwa msimu ujao wa kiangazi. 

Watu wanane waliojitolea watashiriki awamu ya mwanzo ya jaribio hilo, ambapo wanaweza kuongezwa hadi watu 960 ifikapo Desemba. 

Endapo majaribio hayo ya mwanzo yatakuwa yamefanikiwa, hatua ya tatu itahusisha watu 30,000 ambayo imepangwa kufanyika kati ya Aprili na Mei mwakani. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kibaolojia ya Israel, Shmuel Shapira amesema wapo katika hatua ya mwisho. 

Taifa hilo limeripoti visa vipya 674 hapo jana, kutoka katika kilele cha zaidi ya watu 9,000 katika majuma kadhaa yaliopita. Israel pia imeripoti vifo 2,541 vilivyotokana na ugonjwa huo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...