Search This Blog

Saturday, November 21, 2020

India: Pakistani imeumuua mwanajeshi wetu Kashmir


Mwanajeshi wa India ameuwawa na mwengine kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililotokea upande wa Pakistan, kwenye eneo lenye operesheni kubwa ya kijeshi lenye kuligawa jimbo lonalozozaniwa la Kashmir na mataifa hayo mawili hasimu yenye kujihami kwa silaha za nyuklia. 

Msemaji wa jeshi la India, Luteni Kanali Devender Anand anayatuhumu majeshi ya Pakistan kwa kufyatua makombora ya mizinga na silaha nyingine katika maeneo ya udhibiti ya kusini mwa wilaya ya Rajouri.

 Anand amekiita kitendo hicho kuwa ni cha kichokozi na ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano ya 2003 na kusema kwamba jeshi la India walilipiza kisasi. Hata hivyo Pakistan hadi sasa haijasema lolote kufuatia mkasa huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...