Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha jana kuwa Yemen, taifa lililoharibiwa kwa vita limo kwenye hatari ya kutumbukia kwenye baa kubwa la njaa kuwahi kushuhudiwa duniani.
Guterres amesema iwapo hakuna hatua za haraka zitachukuliwa mamilioni ya watu watakufa kwenye nchi hiyo iliyoshuhudia vita ya miaka mitano kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran pamoja na vikosi vya serikali.
Kiongozi hiyo amezitolea wito pande zote zenye ushawishi duniani kuchukua hatua za dharura kuepusha kutokea kwa janga hilo na kuwarai wale wanaohusika na mzozo unaoendelea kujiuzuia na ili kupunguza ugumu wa hali iliyopo.
Guetters ameainisha kuwa sababu zinazotishia kuzuka kwa baa la njaa ni kupungua kwa kiwango kikubwa ufadhili unaotolewa kwa juhudi za msaada wa kiutu wa Umoja wa mataifa, kuanguka kwa sarafu ya Yemen na vikwazo vinavyosababsihwa na pande hasimu.

No comments:
Post a Comment