Search This Blog

Saturday, November 21, 2020

Erdogan azungumza na Mfalme Salman


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa njia ya simu na Mfalme Salman wa Saudi Arabia, kabla ya mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yaliyoendelea na yale yanayoinukia kiuchumi duniani G20. Saudia ndio mwenyeji wa mkutano huo unaofanyika kwa njia ya vidio. 

Kwa mujibu wa ofisi ya rais, viongozi hao wawili wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya mataifa yao mawili. 

Uhusiano kati ya Uturuki na Saudi Arabia ulizorota kwa kiwango kikubwa 2018, baada ya kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi katika ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, na hivyo kuongeza mvutano juu ya uungwaji mkono wa Uturuki kwa kundi la Udugu wa Kiislamu, ambalo serikali ya Riyadh inalitazama kama kundi la kigaidi. L

akini taarifa ya sasa inasema viongozi hao wamekubaliana kufungua milango ya majadiliano na kuboresha uhusiano wa pamoja na kushughulikia masuala kadha wa kadha.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...