Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Mheshimiwa Stephen Lujwahuka Byabato ameapishwa Novemba 10, 2020 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma, na kuwa Mbunge kamili wa Jimbo la Bukoba Mjini tayari kuwatumikia Wanajimbo na Wapiga Kura wake.
Mara kadhaa wakati wa Kampeini Mbunge huyo aliyepewa jina la Entoronyonyo (kitu kisafi/kisichokuwa na Doa), alisikika akiwaomba wapiga Kura kutengeneza Mnara wa Mawasiliano kati ya Rais Magufuli na Jimbo la Bukoba Mjini, ambapo amekuwa akisema Jimbo la Bukoba Mjini kwa Miaka Mitano iliyopita limekosa Mawasiliano mazuri na Rais Magufuli kwani hapakuwa na mnara mzuri wa Mawasiliano (Mbunge) hivyo simu zilikuwa hazipiti.
Mhe. Byabato ambaye ameambatana na Familia yake ameapishwa Rasmi na Wabunge wengine Wateule, muda wa Saa 12:33 Jioni wakati ambapo kiapo hicho awali kilitarajiwa kingefanyika Tarehe 11 Novemba 2020.
Kukamilika kwa kiapo hicho ni kiashiria kwamba Sasa Mheshimiwa Byabato Ni Mbunge Rasmi wa Jimbo la Bukoba Mjini akiwa na Ari na morari ya kuwatumikia Wananchi ailowaomba ridhaa ya Kuwawakilisha Bungeni.
Search This Blog
Tuesday, November 10, 2020
ENTORONYONYO YUPO TAYARI KUUNGANISHA MAWASILIANO BUKOBA MJINI .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment