Rais wa Benki Kuu duniani David Malpass amewaonya viongozi wa mataifa wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G20 kuwa, iwapo watashindwa kuyafuta madeni kwa baadhi ya nchi, basi huenda nchi hizo zikatumbukia katika umaskini mkubwa.
Malpass amesema ameridishwa na maendeleo yaliyofanywa na kundi hilo la G20 juu ya kutoa msamaha wa madeni kwa nchi maskini, lakini hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa.
Rais huyo wa benki kuu duniani amewaambia viongozi hao katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video kuwa kupunguza madeni kwa nchi maskini kutasaidia kuongeza uzalishaji na hivyo basi kuleta afueni ya kudumu kwa mataifa hayo.
Malpass ameonya kuwa changamoto za madeni zinazidi kujitokeza hasa wakati huu wa janga la virusi vya Corona katika mataifa kama vile Chad, Angola, Ethiopia na Zambia na kuwa iwapo mataifa hayo hayatafutiwa madeni yao, basi huenda yakatumbukia katika umaskini.

No comments:
Post a Comment