Askari wawili wa India wameripotiwa kupoteza maisha kwenye mapigano yaliyozuka kati ya vikosi vya usalama na kundi la waasi katika eneo la Jammu Kashmir.
Msemaji wa vikosi vya India Jenerali Rajesh Kalia, alisema kuwa kundi la waasi liwafyatulia risasi askari wa vikosi vya usalama walipokuwa wakishika doria katika maeneo ya mji wa Srinagar.
Msemaji Kalia alipngezea kusema kuwa askari wawili waliojeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo walipelekwa hospitali na baadaye wakafariki.
Vikosi vya usalama vya India vilianzisha operesheni dhidi ya waasi baada ya tukio hilo.

No comments:
Post a Comment