Search This Blog

Tuesday, October 20, 2020

Sirro asema Jeshi la Polisi halijihusishi na siasa

 


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  IGP Simon Sirro, amewahimiza askari wa Jeshi hilo kutimiza wajibu 

Akizungumza na waandishi wa habari  hii leo Oktoba 20,2020,visiwani Zanzibar amesema kazi ya jeshi la polisi ni kuhakikisha wanasimamia sheria na watanzania wanafanya uchaguzi kwa amani ambapo pia amewataka wadau wa uchaguzi kutimiza wajibu wao ipasavyo bila kuvunja sheria.


“Tume ya uchaguzi itimize wajibu wao,viongozi wa siasa watimize wajibu wao na kubwa zaidi nazungumzia hili la kusema kuna baadhi ya kikundi cha watu wamesema watatangaza matokeo hiyo imenishangaza kidogo’’, amesema IGP Sirro.


IGP Sirro ameongeza kuwa viongozi wa siasa wanatakiwa kufuata sheria ambapo pia amewakumbusha kwamba wenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni NEC na ZEC na si mtu mwingine yoyote.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...