Search This Blog

Wednesday, October 14, 2020

Rais Magufuli Amkumbuka Paul Makonda "Mpaka RC Anaomba Mbunge Alikuwa Wapi "


Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli, amesema kuwa mtu wa kwanza aliyeomba ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Ubungo ni aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na ndipo ujenzi huo ulipoanza.

Kauli hiyo ameitoa hii jana Oktoba 13, 2020, wakati akiomba kura kwa wakazi wa Ubungo na Kibamba, ambapo amewataka wasifanye makosa ya kumchanganyia na badala yake wachague madiwani na wabunge kutoka CCM.


“Hospitali ya wilaya ya Ubungo mnakumbuka siku ile tupo kwenye sherehe Airport, iliombwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, mpaka RC anaomba mbunge alikuwa wapi kuomba, tukaijenga kwa sababu Ubungo na Kibamba ilikuwa kama watoto yatima, msiendelee kuwa yatima”, amesema Dkt Magufuli.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...