Search This Blog

Tuesday, October 6, 2020

Mkutano muhimu wa Erdoğan na Stoltenberg


Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mawasiliano, iliarifiwa kuwa masuala ya uhusiano kati ya Uturuki na NATO, pamoja na maendeleo ya Mediterania Mashariki, Syria na Libya yalijadiliwa kwenye mkutano wa Erdoğan na  Stoltenberg .

Erdoğan pia alielezea kuunga mkono mpango wa NATO unaolenga kupunguza mvutano kati ya jeshi la Uturuki na Ugiriki katika eneo la Mediterania ya Mashariki licha ya utata wa Ugiriki hapo awali.

Akikumbushia juhudi za Uturuki za kupambania amani na usalama hasa kipindi cha mzozo wa wahamiaji barani Ulaya,  Erdoğan alisisitiza kuwa NATO pekee ndiyo inayoonyesha ushirikiano katika suala la kurudisha utulivu Libya na kubainisha matarajio ya kuungwa mkono na washirika kwa manufaa na maslahi ya wahusika wote kwa ujumla.

Akitilia mkazo wito wa kusitisha mzozo na kuondolewa kwa Waarmenia waliovamia ardhi ya Azerbaijan kufuatia uamuzi wa Baraza la Usalama la UN likishirikiana na Shirika la Usalama wa Ulaya, Erdoğan alibainisha kuwepo kwa baadhi ya washirika wa NATO wanaounga mkono makundi ya kigaidi ya PKK/PYD/YPG pamoja na kushirikiana na wanachama wa FETÖ.

Rais Erdoğan aliashiria mshikamano thabiti unaohitaji kuwepo kati ya washirika wa NATO na Uturuki ambao una umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya muungano huo, na kupunguza athari mbaya ya utendaji kazi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...