Waziri anayeshughulika na mkataba wa kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya almaarufu Brexit, Michael Gove, amesema leo kwamba Uingereza ''imejiandaa vizuri'' kwa kuondoka katika Umoja huo bila ya mkataba.
Katika nakala kupitia jarida la Sunday Times , Gove amesema kuwa hali hiyo sio anayopendelea lakini kama chaguo ni kati ya mpangilio unaowafunga kwa muda usiojulikana ama pale wanapoweza kujipangia mwelekeo wao wa siku zijazo, basi hakuna chaguo hapo.
Ameongeza kuwa kuondoka kwa matakwa ya Australia ni matokeo ambayo wamejipanga nayo.

No comments:
Post a Comment