Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu ameahidi kusukuma upatikanaji wa Umeme wa Rea na Kuboresha Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari katika kata ya Marungu.
Ummy akiinadi Ilani ya Ccm na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Kata ya Marungu iliyo pembezoni mwa Jiji la Tanga, amesema Ilani ya Ccm imeeleza kufikisha umeme katika maeneo ya pembezoni kupitia kwakutumia REA (Mpango wa Umeme Vijijini)hivyo endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha maeneo ya Amani,Mkembe na Marungu yanapata umeme wa Rea ambao ni nafuu kwa wananchi ili maeneo hayo yafunguke Kibiashara kwa watu kujiajiri kwenye shughuli mbalimbali.
Aidha Ummy ameeleza pia umuhimu wa kuboresha Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari ili iwe Rafiki kwa watoto kusoma na hatimae kutimiza ndoto zao pasipo vikwazo”Mimi najua hapa Marungu kuna watoto wana akili sana tukiwaboreshea mazingira ya Shule zao watasoma vizuri na tutapata Madaktari,Wanasheria kama mimi na hata Marubani Ndugu zangu niamini nitafanya maboresho makubwa kwenye shule zetu .Amesema Ummy Mwalimu”.
Search This Blog
Wednesday, October 14, 2020
MGOMBEA UBUNGE TANGA MJINI AAHIDI UPATIKANAJI UMEME WA REA NA UBORESHAJI MIUNDOMBINU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...





No comments:
Post a Comment