Maofisa 5 akiwemo Kamanda wa Wilaya wameachishwa kazi wakituhumiwa kuharibu ushahidi wa tukio la binti wa miaka 19 kubakwa na kuuawa na kundi la wahuni jambo lililosababisha maandamano ya watu
Polisi hao wanatuhumiwa kuchelewesha usajili wa kesi pamoja na malalamiko ya ndugu wa marehemu na pia walifanya maamuzi ya kuuchoma mwili wa marehemu bila ridhaa ya familia yake
Aidha, Polisi wamekosolewa na jamii wakidaiwa kuvizuia Vyombo vya Habari na Vyama vya Siasa vya Upinzani kuongea na familia ya marehemu
Marehemu alifanyiwa ukatili huo na wanaume 4 katika eneo lililo karibu na kijiji alichokuwa anaishi Kaskazini mwa #India
No comments:
Post a Comment