Search This Blog

Sunday, October 4, 2020

Magufuli akiri kufahamu changamoto za Muungano

 



Na Thabit Madai, Zanzibar.

Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli amesema anazifahamu changamoto ndogondogo za muungano zilizopo na hashindwi kuzitafutia ufumbuzi akiwa pamoja na Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa ngazi ya Urais.

Magufuli amesema nia yake yakugombea tena nafasi hiyo nikuhakikisha mapinduzi ya  mwaka 1964 ya  Zanzibar na Muungano Vinaendelea kudumu kwa maendeleo ya vizazi Vijavyo.

Akiwahutubia wanaccm na  wananchi wa Zanzibar waliofurika katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja ambapo kwanza ana aza hutuba yake kwa kusifia utekelezaji wa ilani ya ccm kwa upande wa Zanzibar iliyosimamiwa na Dk. Ali Mohammed Shein.

Aidha aliwataka wazanzibari kumchagua Dk. Mwiniyi ili kwa upande wa Zanzibar na yeye kwa Upande wa Tanzania bara ili kuhakikisha kelele za wapinzani juu ya muungano zinamalizwa baada ya Uchaguzi wa October 28.

Hata alisema akizungumzia maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano na ijayo ya Zanzibar Dk. Magufuli amesema serikali imepanga kununua meli nne za uvuvi ,pamoja nakuweka mazingira bora ya yakibiashara.

Mapema  Dk. Ali Mohammed alisema hana shaka na kura za  mgombea urais wamuungano Dk. John Pombe Magufuli kutokana na mema aliyoyafanya kwa upande wa  wazanzibar.

Kwa upande wake mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwaomba kura wazanzibar ametaja baadhi ya miradi aliyoomba msaada toka kwa serikali ya jamuhuri ya mungano ambo itatekelezwa katika awamu ijao.

Mkutano huu wa kampeni ulihudhuriwa na wanachi wa mikoa mitatu ya Zanzibar,ambapo wasanii mbali mbali walipamba mkutano huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...