Search This Blog

Thursday, October 22, 2020

Kamati ya amani yakutana Njombe,waweka mkakati wa kutunza amani


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wadau mbali mbali na viongozi wakiwemo viongozi wadini,wa mila,serikali pamoja na jeshi la polisi,wamekutana kwa pamoja ili kuweka mikakati ya kutunza amani kabla na baada ya uchaguzi.

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ndiye mgeni rasmi aliyefungua mkutano wa amani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.

Hoja mbali mbali zimejadiliwa baina ya viongozi wa dini,viongozi  wa mila,jeshi la polisi,serikali pamoja Elimu kwa mpiga kura kutoka kwa mratibu wa uchaguzi mkoa wa Njombe ili viongozi hao wanaoishi na jamii kwenda kushiriki kikamilifu katika zoezi la kushirikisha jamii dhidi ya umuhimu wa kutunza amani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...