Timu ya Miami Heat imeibuka na ushindi wa pointi 104-115 dhidi ya timu ya LA Lakers, katika mchezo wa tatu wa fainali za NBA.
Butler sasa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kufunga pointi 40 na triple-double kwenye fainali za NBA. Wachezaji wengine ambao wamewahi kufanya hivyo ni LeBron James na Jerry West ambaye kwasasa ni miongoni mwa maofisa wa NBA.
Nyota wa Lakers LeBron James alimaliza mchezo huo akiwa na pointi 25, assists 8 na rebounds 10.
Ushindi huo wa Miami Heat umefanya matokeo kuwa 2-1 Lakers wakiongoza series.
Mchezo wa nne wa fainali hizo utapigwa kesho Jumanne Oktoba 6, 2020.

No comments:
Post a Comment