Wakati kampeni zinaelekea ukingoni leo tarehe 21.10.2020 mgombea wa nafasi ya Ubunge jimbo la kisarawe Mhe Selemani Jafo alikuwa katika kata ya Mzenga kijiji cha Mitengwe(Paris)
Akifanya muendelezo wa kampeni zake leo Jafo amewafundisha na kuwaelekeza wakazi wa mzenga jinsi ya kupigia kura wagombea wote wa CCM " Unapoenda kupiga kura hakikisha unampigia kura Rais kwenye boksi nambari moja, Utanipigia na mimi kwenye boksi nambari mbili pia utamchagua na diwani kulingana na kata husika , hivyo niwaombe sana tena sana wanakisarawe ifikapo oktoba 28 tusifanye makosa, tuichague CCM" Alisema Jafo
Hata hivyo Jafo hakuishia hapo aliendelea kutoa ahadi mbalimbali ikiwemo ujenzi na Ukarabati wa barabara, ameahidi kutatua kero ya maji katika kata ya Mzenga, ameahidi kusaidia vikundi vya akina mama,wazee,vijana na Walemavu kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba ili kujikwamua kiuchumi, ameahidi pia ujaziliziaji wa umeme katika maeneo ambayo hayana umeme.
Aidha mgombea huyo aliendelea kuinadi ilani ya chama cha mapinduzi ili kuwaaminisha wanakisarawe kuwa kila anachoahidi kipo ndani ya ilani ya chama na ni lazima kitekelezwe,
Jafo pia alikiombea kura chama chake cha CCM na kuwataka wanamzenga kuwapigia kura wagombea wote kupitia CCM ambao ni Rais, Mbunge na Diwani.
Pia katika kampeni hizo mke wa Mhe jafo alitumia nafasi hiyo kumuombea kura mume wake
" wanakisarawe Jafo anawapenda Sana, mda mwingi anawaza kuhusu kisarawe, mimi binafsi kuna wakati nakosa nafasi ya kuwa na mume wangu yote ni jinsi gani anavyowapenda, yupo radhi asile asilale ili afanye kazi kwa ajari ya kisarawe, Naombeni sana mumpe kura za ndio ifikapo oktoba 28, si yeye peke ake ni pamoja na mgombea Uraisi Mhe John Magufuli na wagombea udiwani wote katika Jimbo la kisarawe" alimaliza bi Rahma
Hata hivyo Jafo hakuacha kusisitiza amani " Naombeni vijana tuendelee kudumisha amani yetu,tusitumike katika kuleta fujo, tulinde amani yetu na mungu atatusimamia katika hili" Alimaliza Jafo.

No comments:
Post a Comment