Kundi la kwanza la mahujaji Waislamu liliwasili katika eneo takatifu zaidi nchini Saudi Arabia hii leo kufanya ibada ndogo ya hija inayojulikana kama Umrah, miezi saba baada ya ibada hiyo kusimamishwa kwa sababu ya mripuko wa virusi vya corona.
Karibu mahujaji 6,000 wanaoishi ndani ya Saudi Arabia wanaruhusiwa kwa siku kuingia katika msikiti mkubwa mjini Mecca kufanya ibada ya Umra chini ya utaratibu unaolenga kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.
Picha kwenye vyombo vya habari nchini Saudi Arabia zilionyesha mahujaji wakiwa wamevaa barakoa na kudumisha utaratibu wa watu kutosogeleana wakati walipokuwa wakizunguka jengo takatifu la Kaaba lenye umbo la mchemraba ndani ya msikiti huo.
Waislamu kutoka nje ya nchi hiyo wataruhusiwa kuanza kuelekea katika taifa hilo la kifalme kwa hija ya Umrah kutoka Novemba 1, wakati mahujaji 20,000 kwa siku wataruhusiwa kuingia katika msikiti huo.

No comments:
Post a Comment