Search This Blog

Sunday, October 25, 2020

DC Kyobya: ”TBS watembeleeni wafanyabiashara wadogowadogo ili waweze kupata vibali”


 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Wito umetolewa kwa Shirika la viwango Tanznaia (TBS) Wilayani Mtwara kuwatembelea wafanyabiashara wadogowadogo ili kutambua na kupata vibali ili bidhaa zao ziweze kutambulika.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara  Dunstani Kyobya alipotembelea maonesho ya mabanda ya biashara ya akina mama yanayofanyika viwanja vya Mashujaa Park vilivyopo manispaa Mtwara Mikindani.


Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa na ni vyema kwa TBS wakatenga muda wa kuwatembelea akina mama wanaotengeneza bidhaa kwa  kutumia mikono yao ili waweze kufahamu namna ya kupaata vibali vya TBS na bidhaa zao ziweze kuuzaika maeneo tofauti tofauti.

Aidha amechukua fursa hiyo kwa kuwasihii akina hao kutengeza vikundi vya kutosha ili waweze kupata mikopo inayotolewa kwa Halmshauri zote hapa nchini.

Lakini pia Mkuu huyo wa Wilaya amewasihii akina mama hao kutimia mikopo kwa kuongeza mitaji yao ili waweze kupata fedha za marejesho na sio matumizi ambayo mwisho wa siku itawaghalimu kwenye marejesho.

“Akina mama tengenezeni vikundi mvisajili nendeni kwa mkurugenzi mkachukue mikopo,Wlaya yangu ina Halmashauri tatu ,kuna hapa mjini ,kunan vijijini na Nanyamba na huko tunatoa mikopo”

Mkuu huyo wa Wilaya amewasisitiza akina mama hao kuongeza thamani ya bidhaa zao ili ziweze kuuzuka ndani na nje ya nchi pia.  



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...