Search This Blog
Monday, October 19, 2020
Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye..Nifanyeje?
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.
Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.
Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo sio mshamba kama huyu wa zamani.
Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment