Search This Blog
Wednesday, September 9, 2020
Yafahamu Majimbo ambayo NEC imeyatolea maamuzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imezipitia, kuzichambua na kuzifanyia maamuzi rufaa 34, ambazo kati ya hizo imekubali rufaa 13 na kuwarejesha wagombea wa majimbo 9 na imekataa rufaa 7 za wagombea ambao hawakuteuliwa, huku pia ikikataa rufaa 14 za kupinga walioteuliwa.
Taarifa hiyo imetolewa hii leo Septemba 9, 2020, na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt Wilson Mahera, ambapo ameyataja majina ya majimbo ambayo rufaa 13 imezikubali ikiwemo Singida Magharibi, Madaba, Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene na Kigamboni.
Aidha mbali na kukubali rufaa hizo 13, pia imekataa rufaa 7 za wagombea ambao hawakuteuliwa, rufaa hizo ni kutoka kwenye Majimbo ya Singida Magharibi, Bahi, Handeni Vijijini, Madaba, Singida Mashariki, Ileje, Meatu na Bukene.
Mbali na hizo NEC pia imekataa rufaa 14, za kupinga walioteuliwa kutoka katika majimbo ya Igunga, Mwanga, Mafinga, Ilala, Manonga na Kisesa.
Idadi hiyo ya leo inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 89, Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku na wahusika wa rufaa hizo watajulishwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment