Search This Blog

Wednesday, September 9, 2020

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki kufanya ziara Ukanda wa Afrika Magharibi


Mevlüt Çavuşoğlu waziri wa mambo ya nje wa  Uturuki atarajiwa kufanya ziara rasmi katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Ziara yake hiyo waziri wa mambo ya nje wa Uturuki atajielekeza nchini Mali, Senegal na Guinea Bisau.

Ziara hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Uturuki itachukuwa muda wa siku tatu kuanzia  Septemba 9 hadi Septemba  11.

Masuala tofuati katika ushirikiano uliopo kati ya Uturuki na mataifa hayo katika ukanda wa Afrika Magharibi  yatajadiliwa.

Taarifa iliotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imefahamisha kwamba suala zima kuhusu uwekezaji, usalama ushirikiano wa kidiplomasia na maendelea  CEDEAO ndio masuala muhimu ambayo yatazungumziwa katika ziara ya awaziri wa mambo ya nje wa Uturuki na viongozi tofauti katika Ukanda huo.

Imearifiwa kuwa ziara ya waziriwa mambo ya nje wa Uturuki nchini Senegal na Ginea  Septemba 10 ndio itakuwa ziara yake ya kwanza katika mataifa hayo kama waziri wa mambo ya nje.

Masuala tofauti ya ushirikiano kati ya Uturuki na mataifa hayo pia yatajadiliwa ikiwemo pia masuala ya kimataifa.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...