Search This Blog

Wednesday, September 23, 2020

Waziri Kabudi: Serikali haikuwa na lengo la kuvizuia vyombo vya habari vya kimataifa


 Waziri wa Mambo ya Nje. Prof. Palamagamba Kabudi amezungumzia suala ya Vyombo vya Habari vya Kimataifa vinavyotaka kutumia vyombo vya hapa nchini kurusha matangazo kuomba leseni na kusema Serikali haikuwa na lengo la kuvizuia kuendesha vipindi vyake

Amesema lengo lake ni kutambua vyombo hivyo vinashirikiana na vyombo gani vya Tanzania, na hadi sasa vyombo vyote vya kimataifa vimeshatekeleza agizo hilo na kupata leseni

Vilevile, amezungumzia mabadiliko ya Sheria za Asasi za Kiraia na Vyama vya Siasa yanalenga kuongeza uwazi na uwajibikaji katika fedha zinazoingia kwaajili ya miradi pamoja na matumizi yake

Ameeleza kuwa, hatua hiyo inaendana na Sheria na Taratibu za Kimataifa za kuzuia utakatishaji fedha ili kuhakikisha makundi yenye nia ovu hayatumii njia hizo kuingiza fedha zao




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...