Uingiliaji wa vikosi vya usalama katika maandamano ya "Ijumaa ya Hasira" huko Misri, umepelekea watu 3 kupoteza maisha huko Giza.
Wanaharakati wa upinzani wa Misri na vyombo vya habari vimetangaza kuwa watu 3 wamefariki huko Giza kutokana na uingiliaji wa polisi katika maandamano ya "Ijumaa ya Hasira" yaliyofanyika jana.
Katika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter, Mohammed Ali mpinzani wa Misri, anayeishi Uhispania, amesema,
"Licha ya maandamano ya amani, Wizara ya Mambo ya Ndani (wilaya ya Giza) imewaua watu 3 huko El-Iyad."
Televisheni ya "Vatan" yenye uhusiano na Jumuiya ya Udugu wa Kiislamu (Ikhwan) imetangaza kuwa watu watatu, Sami Vefdi Seyid Bashir, Riza Muhammed Hamid Abu Imam na Muhammad Nasir Hamdi Ismail, wamefariki kutokana na kuingilia kati kwa vikosi vya usalama.
Utawala wa Misri haujatoa tamko juu ya suala hilo bado.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Misri waliuita umma uingie barabarani kwa wingi katika maandamano dhidi ya serikali "Ijumaa ya Hasira" yaliyopangwa kufanyika jana.

No comments:
Post a Comment