Search This Blog

Monday, September 21, 2020

TAWA YAANZA KUUZA NYAMA ZA WANYAMAPOLI KWENYE BUCHA ZILIZO CHINI YA MAMLAKA HIYO

Kamishna wa Wanyamapori Kamishna Mabula Misingwi 

********************************* 

NA FARIDA SAIDY, MOROGORO. 

Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Nchini (TAWA) imeanzisha utaratibu wa kuuza nyama za wanyamapori kwenye Bucha zilizo chini ya Mamlaka hiyo ili kutoa fursa kwa kila Mwananchi aweze ya kutumia kitoweo hicho. 

Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna wa Wanyamapori Kamishna Mabula Misingwi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani morogoro ambapo amesema tangu kutolewa kwa agizo hilo wamekuwa wakifanya tahmini kuhusu taratibu utakao tumika kuuza nyama hizo. 

Hata hivyo ameendelea kusema kuwa katika kurudisha faida kwa wananchi TAWA imeanzisha miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa ufugaji nyuki ambao unazalisha tani 1000 za asali na zaidi ya vikundi 58 na wanachama 268 wamenufaika na mradi huo. 

Katika hatua nyingine amesema ili kupunguza uvamizi unaofanywa na wanyamapori katika maeneo ya makazi na mshamba hapa nchini,amewashauri Wananchi kuishi katika maeneo yaliorasimishwa kwa makazi ili kujilinda na wanyama wakali na waharibifu wanaotoka katika mbuga za wanyama na hifadhi za Taifa. 

Hata hivyo amesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuthamini, kulinda na kudhibiti ujangili wa wanyamapori walio karibu na maeneo yao, ambapo mpaka sasa club 163 zimeanzishwa katika shule za msingi kwa lengo la kuwapatia elimu namna ya kuweza kuepukana na wanyama wakali na waharibifu.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...