Taasisi za serikali hasa zenye nguvu kazi za kutosha na ambazo zipo kwenye maeneo yanayozalisha korosho zimeshauriwa ziangalie uwezekano wa kuanzisha viwanda vidogo vya kubangua korosho.
Wito huo wenye lengo la kuliongezea thamani zao hilo ulitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wakati wa hafla ya kukabidhi mashine mbili za kubangua korosho kwa chuo kikuu cha Stella Marins, ambazo zimetengenezwa na SIDO.
Ndemanga alisema ili kuliongezea thamani zao hilo na kuepukanana ubabaishaji wa wanunuzi wa korosho ghafi kuna haja ya kuongeza uwezo wa kubangua korosho hapa hapa nchini badala ya kuuza zikiwa ghafi.
Alisema kwakufanya hivyo zao hilo litakuwa na uhakika wa kuwa na soko la ndani. Kwani kuna mahitaji makubwa ya korosho zilizobanguliwa ikilinganishwa na kiwango cha Korosho zinazobanguliwa na kuuzwa kwa walaji wa ndani.
Katika kuhakikisha azima hiyo inafikiwa, Ndemanga ambaye aliyasema hayo kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Lindi alisema kuna haja ya taasisi za serikali ikiwamo magereza ambazo zipo katika maeneo yanayozalisha zao hilo ziangalie uwezekano wa kuanzisha viwanda vya kubangua zao hilo.
" Nakupongeza kamanda wa magereza wa mkoa wa Mtwara kwa wazo zuri la kuanzisha kiwanda chenu cha kubangua korosho katika gereza la mkoa na tayari mmeshalipa fedha kwani SIDO, ni jambo jema. Kwahiyo korosho mnazozalisha mtakuwa mmeziongezea thamani. Ni vema sasa taasisi nyingine za serikali ziangalie uwezekano wa kuanzisha viwanda," Ndemanga alipongeza na kutoa wito.
Katika hali inayodhihirisha mwakilishi huyo wa mkuu wa mkoa wa Lindi kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za SIDO mkoa wa Lindi amedhamiria taasisi za serikali zenye uwezo wa kuanzisha viwanda hivyo zianzishe, alitoa wito kwa halmashauri zilizopo mkoani Lindi ziangalie uwezekano wa fedha zinazokopeshwa kwa vikundi vya wajasiriamali zielekezwe katika kuanzisha viwanda.
Alisema licha ya halmashauri kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali lakini miradi mingi ya vikundi hivyo haiendelei. Nabaadhi ya vikundi havitumii fedha hizo kwa ajili ya shughuli zinazolengwa. Kwahiyo ni vema halmashauri zikavitupia jicho vikundi vinavyolenga kuanzisha viwanda vidogo.
Ndemanga pia alitoa wito kwa SIDO ifuatilie matumizi ya mashine inazotoa kwa wateja wake ili iweze kujua zina uwezo wa kufanya kazi kwakiasi gani na kama zinakasoro ziweze kurekebishwa. Kwani miongoni mwa wajibu wa shirika hilo nikusambaza teknolojia. Kwahiyo halinabudi kufuatilia ili kujiridhisha kama teknolojia hizo zinafanyakazi kama ilivyokusudiwa.
Alishauri maofisa wa shirika hilo waende kwa wakulima wa korosho ili kuwahamasisha wanunue mashine za kubangua Korosho. Kwani wakulima wengi wa zao hilo wanauwezo wa kununua mashine hizo na kuanzisha viwanda.
" Uhakiki uliofanyika kwa wakulima wa korosho umeonesha wakulima wengi wanapata fedha nyingi kutokanana uzalishaji wanaofanya. Baadhi yao wanapata zaidi ya shilingi milioni miatatu. Mashine hizi mbili mnauza shilingi milioni hamsini na Saba tu. Niaibu kwamkulima wa aina hiyo kushindwa kununua na kuanzisha kiwanda chake," Ndemanga alisisitiza.
Kwaupande wake meneja wa SIDO wa Mkoa wa Lindi, Mwita Kasisi alisema shirika hilo linajitahidi kupeleka teknolojia kwa wananchi. Kwani ni miongoni mwa wajibu wake wamsingi. Huku likijitahidi kuhakikisha bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vidogo zinapata masoko. Kwahiyo inalojukumu jingine la kuhakikisha bidhaa hizo zinakuwa bora.
Aidha meneja huyo alisema serikali inaweka fedha nyingi kwenye shirika hilo ili wenye uhitaji wa kukopa kwa ajili ya mitaji waweze kukopeshwa. Ambapo wateja wenye uhitaji wa fedha nyingi kuliko viwango vinavyotelewa na shirika hilo, wanaongozwa na kusaidiwa njia za kupata mikopo wenye taasisi za fedha.

No comments:
Post a Comment