Search This Blog

Sunday, September 27, 2020

Rais Macron asema Lukashenko anatakiwa kuondoka

 


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema ni wazi kwamba rais wa Belarus Alexander Lukashenko anatakiwa kuondoka. 

Macron alikuwa akizungumza na gazeti la wiki la Ufaransa la Journal Dimanche, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la AFP. 

Macron alinukuliwa akisema, ni mzozo wa kimamlaka na utawala wa kiimla ambao haukubaliani na misingi ya kidemokrasia na ambao unashikiliwa kwa kutumia nguvu na kuongeza kuwa ni wazi Lukashenko anatakiwa kuondoka. 

Matamshi hayo ya Macron yanakuja siku chache baada ya Umoja wa Ulaya kuchapisha taarifa iliyoibua upya madai kwamba uchaguzi wa Belarus wa Agosti 9 haukuwa huru wala wa haki na kutomtambua Lukashenko kama rais wa taifa hilo.

Katika hatua nyingine nchini Belarus maelfu ya wanawake waliandamana jana mjini Minsk wakimpinga rais huyo na kulingana na kundi la haki za binaadamu la Viasna kiasi watu 60 walikamatwa ikiwa ni pamoja na mwanaharakati wa muda mrefu Nina Baginskaya.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...