Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan, ameionya Ugiriki kuingia katika mazungumzo kuhusu eneo linalozozaniwa la mashariki mwa bahari Mediterrania, au waathiriwe.
Akizungumza katika hafla ya kufungua hospitali mjini Istanbul, Erdogan amesema, Ugiriki italazimika kuelewa lugha ya siasa na diplomasia au uwanjani kwa madhara machungu.
Uturuki inazozana na Ugiriki pamoja na Cyprus kuhusu haki za kutafuta gesi na mafuta mashaeriki mwa bahari Mediterrania.
Pande zote kwenye mvutano huo zimepeleka vikosi vya jeshi vya majini na angani kutetea madai yao katika eneo hilo.
Hayo yakijiri, gazeti la Cumhuriyet la Uturuki limeripoti kuwa vifaru 40 vya kijeshi vimekuwa vikisafirishwa kutoka mpaka wa Syria kuelekea Edirne, kaskazini magharibi mwa Uturuki.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment