Search This Blog

Wednesday, September 16, 2020

PICHA: Mgombea Urais Wa CCM Dkt Magufuli Awatuza Kofia Wasanii Kala Jeremiah Na Ali Kiba Katika Mikutano Ya Kampeni Bukoba Na Biharamulo

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kofia msanii Ali Kiba baada ya kutumbuiza katika Mkutano wa Kampeni mjini Bukoba mkoani Kagera jana Jumatano Septemba 16, 2020. 

Rais Dkt. Magufuli ameitaja Sanaa kama moja ya sekta muhimu sana za uchumi nchini na kuahidi kuisimamia kikamilifu katika kipindi chake cha pili cha Serikali ya awamu ya Tano endapo akichaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa miaka mitano mingine.
Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kofia msanii Kala Jeremiah baada ya kutumbuiza katika Mkutano wa Kampeni mjini Biharamulo mkoani Kagera leo Jumatano Septemba 16, 2020.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...