Search This Blog
Wednesday, September 9, 2020
NEC Yafanyia Maamuzi RUFAA Mapingamizi 55
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa uamuzi wa rufaa 55 za wagombea Ubunge ambapo, imekubali rufaa 15 za Wagombea Ubunge na kuwarejesha katika orodha ya wagombea na imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa na pia imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.
Taarifa hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera na kusema kuwa zoezi la kuzijadili na kuzitolea uamuzi rufaa hizo litaendelea, na hivyo Tume itakuwa inatoa uamuzi na kuwajulisha wahusika kwa kadri rufaa hizo zitakuwa zinamalizika kushughulikiwa.
Aidha Dkt Mahera ameongeza kuwa Tume hiyo imechambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa, vilivyowasilishwa ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi na wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kwa njia ya barua juu ya uamuzi wa Tume kuanzia leo Septemba 8, 2020.
Septemba Mosi, 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilitangaza kuanza kusikiliza Rufaa 557 zilizokatwa na wagombea wa ngazi za Ubunge na Udiwani kutoka Majimbo mbalimbali nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment