Search This Blog

Thursday, September 24, 2020

Ndejembi azidi kuzisaka kura, Aahidi kumaliza changamoto ya Maji Chamwino


Kampeni za Ubunge Jimbo la Chamwino ambapo mgombea wake Deo Ndejembi wa Chama cha Mapinduzi  zimeendelea leo kwenye kata ya Haneti ambapo mgeni rasmi alikua Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa huku pia zikihudhuriwa na Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile.

" Ndugu zangu wa Haneti nimekuja mbele yenu kuomba kura za Mgombea wetu wa Urais, Dk John Magufuli, zangu mwenyewe nafahamu Diwani wetu Abdi Mohammed ameshapita bila kupingwa, Oktoba 28 twendeni mkatuchague ili tuweze kuharakisha maendeleo kwa kasi na haraka zaidi.

Haneti mna changamoto ya Maji, mna changamoto ya miundombinu ya barabara, mimi kijana wenu nina uwezo na nguvu ya kuwatumikia na kutatua changamoto zenu, naomba mniamini nikawafanyie kazi na Chamwino iwe na hadhi kweli ya kuwa na Ikulu.

Rais Magufuli amefanya mambo makubwa hapa Haneti, leo umeme unawaka kwa sababu yake, leo akina Mama mnafanya biashara mwaka mzima bila kusumbuliwa na mtu kwa kulipia kitambulisho cha mjasiriamali ambacho ni 20,000 tu, Ichagueni CCM tena na Rais Magufuli ili tuzidi kupaa zaidi," Deo Ndejembi.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...