Search This Blog

Saturday, September 5, 2020

Mgombea ubunge jimbo la Lindi kupitia ACT-Wazalendo ataja atakayoanza nayo



Na Ahmad Mmow, Lindi

Mgombea ubunge katika jimbo la Lindi kupitia Chama cha Alliance for Change Transparency (ACT-Wazalendo), Isihaka Mchinjita amehaidi kuanza kushughulikia sekta ya elimu, uvuvi na kilimo iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Mchinjita ametoa ahadi hiyo leo katika mtaa wa Mnazimoja, manispaa ya Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ubunge jimbo la Lindi.

Mchinjita ambae ni mwalimu alisema anatambua kwamba jimbo hilo linachangamoto nyingi. Hatahivyo akichaguliwa na kuwa mbunge ataanza kushughulikia changamoto zilizopo kwenye sekta za kilimo, uvuvi na elimu.

Alisema wananchi wengi wa jimbo hilo wanategemea kilimo na uvuvi ili kujipatia vipato. Hata hivyo sekta hizo haziwanufaishi kutokana na usimamizi usioridhisha ambao unasababisha wananchi wawe na vipato duni ambavyo havifavilingani na kazi kubwa wanazofanya.

Alisema wakulima hawalipwi bei za kuridhisha wanapouza mazao yao, kwani wanadhulumiwa. Huku akisema hata sekta ya uvuvi imehujumiwa nakusababisha maisha ya wavuvi kuwa magumu ingawa wanafanyakazi ngumu.

Kuhusu sekta ya elimu, mgombea huyo alisema jimbo hilo linahuaba wa shule za msingi na sekondari. Hali inayotokana na waliokuwa wabunge wajimbo hilo kutotambua umuhimu wa elimu kwa maisha na maendeleo ya wananchi.

Alisema jimbo hilo linamitaa takribani 137. Hata hivyo lina shule za msingi 133. Hali inayosababisha baadhi ya watoto kutembea umbali mrefu kwenda ziliko shule. Huku akiongeza kusema kwamba jimbo hilo lina shule za sekondari kumi tu.

" Hata shule ya sekondari ya Lindi ambayo baadhi ya majengo yake yaliungua moto haijakarabatiwa licha ya michango iliyofanyika nakufanikisha kukusanya takribani shilingi milioni mia nane. Kuwanyima watu elimu nisawa na kuuwa maarifa ya kizazi husika,"  alisema Mchinjita.

Mbali na hayo Mchinjita alilaumu kutokamilika mradi wa mtambo wa kuchakata gesi asilia( NLG) ambao unatarajiwa kujengwa katika manispaa ya Lindi. Kwani mtambo huo ungeweza kutoa ajira takribani 5,000 ambazo zingesababisha mzunguko mkubwa wa fedha kwa wananchi wa jimbo hilo na mkoa wa Lindi.

Alibainisha kwamba mji wa Lindi hauna harakati za kiuchumi zenye tija na umedorora. Kwani shughuli zimekuwa ngumu kutokana na kutokuwa na viwanda ambavyo wafanyakazi na vibarua wa viwanda wangeweza kununua bidhaa za madukani, vyakula kungekuwa na wageni wengi ambao wangelala kwenye nyumba za kulala wageni. Hata hivyo kwasasa biashara zote hizo ni ngumu.

Mgombea huyo alikwenda mbali kwakusema hana uhakika kama mradi huo utakamilika. Nikutokana na kutozungumzwa kama ilivyokuwa awali. Ambapo wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara walitaraji wangenufaika na ugunduzi wa gesi asilia iliyogunduliwa katika mikoa hiyo.

" Gesi asilia ambayo tuliaminishwa ingekuwa ni mkombozi wa uchumi wa mikoa hii haizungumzwi tena. Badala yake inazungumzwa miradi ya reli, barabara za juu na ndege ambayo haina faida ya moja kwa moja kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara," alisema Mchinjita.

Alisema kuachanana mradi wa gesi kuna hasara kwa wananchi wa mikoa hiyo ambao waliamini ndani ya miaka mitano baada ya ugunduzi huo wangekuwa na uchumi nzuri ambao ungetokana na gesi hiyo ambayo alisema ugunduzi wake unaashiria kuwepo mafuta.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...